Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamati ya Bunge ya Viwanda yataja maeneo manne ya kufanyiwa kazi

57498 PIC+KAMATI

Wed, 15 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeyataja maeneo manne waliyoshauri katika bajeti ya mwaka 2018/19 ambayo haikuridhishwa na utekelezaji wake.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 14 2019 na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Kanali Mstaafu Masoud Ali Khamis wakati akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Mazingira 2019/2020.

“Serikali kuendelea kuchukua hatua kwa wawekezaji ambao bado hawajaitikia wito wa kufufua viwanda vilivyobinafsishwa,”amesema ni miongoni mwa maeneo ambayo hawajaridhishwa nayo.

Ametaja eneo jingine ni kuangalia namna ya kuunda tume maalum itakayofuatilia eneo la viwanda vilivyobinafsishwa kwa lengo la kufuatilia kwa  ukaribu na kujua ukweli wa eneo hilo. 

Khamis ametaja eneo jingine kuwa ni jitihada za makusudi ziendelee kuchukuliwa katika kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuwavutia wawekezaji wengi.

“Serikali kuendelea na juhudi za kuziwezesha taasisi zake za utafiti ikiwemo Camartec, Sido, Tirdo na Temdo ili ziweze kubuni zana mbalimbali za kilimo zitakazosaidia na kumrahisishia mkulima kuendeleza shughuli zake kwa urahisi ukizingatia kilimo ndio shughuli kuu ya Watanzania walio wengi,”amesema.

Pia Soma

Mwisho

Chanzo: mwananchi.co.tz