Dodoma. Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dk Medard Kalemani amesema sekta ya madini inachangia asilimia 80 ya uzalishaji wa umeme nchini.
Amesema asilimia 56 ya umeme unaozalishwa unatokana na gesi.
Kalemani ametoa kauli hiyo leo Jumatano Novemba 6, 2019 katika maonyesho ya wiki ya asasi zisizo za kiserikali (Azaki) jijini Dodoma.
Amesema gesi ilipogunduliwa mara ya kwanza nchini ilikuwa na futi za ujazo mbili tu lakini mpaka sasa kuna futi za ujazo 57.54 trilioni na tayari baadhi ya maeneo imeanza kutumika.
"Kwa hiyo sekta ya gesi ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Mpaka sasa tumetenga kiasi cha gesi futi za unazo 5.64 trilion kwa ajili ya matumizi ya viwandani na kusambaza majumbani.”
“Kuna mabomba manne na wananchi 500 wameshaunganishiwa umeme wa majumbani na nyingine zinatumika kwenye magari badala ya mafuta ya dizeli na petroli,” amesema Kalemani.