Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kairuki awapa maagizo TTB

Kairuki Pic Kairuki awapa maagizo TTB

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ameitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujipambanua ili kuhakikisha inatekeleza majukumu yake ipasavyo na kukua katika utangazaji utalii. - Ameyasema hayo leo Desemba 13,2023 jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi katika Makao Makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania. - “Tunatamani tuache alama , nataka shirika hili liende mbele katika utangazaji utalii” Waziri Kairuki amesisitiza. - Ameitaka menejimenti ya bodi hiyo kujifanyia tathmini ili kujua ni kipi kinatakiwa kutekelezwa katika kutangaza utalii wa Tanzania hasa kupitia Wakurugenzi waliostaafu. - Pia, ameitaka bodi hiyo kujenga utaratibu wa kuwasiliana na kushirikiana na balozi mbalimbali za Tanzania zilizopo nje ya nchi kwa kuwapatia taarifa muhimu za kutangaza utalii. - Kuhusu ustawi wa Watumishi Waziri Kairuki ameahidi kufanyia kazi changamoto zinazowakabili ili kuhakikisha shirika hilo linafanya kazi ipasavyo na kuwaasa Watumishi wa Bodi hiyo kuwa na utaratibu wa kujiendeleza kielimu ili kuendana na teknolojia hasa katika masuala ya utangazaji utalii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live