Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kairuki aeleza sababu wawekezaji kutimka

56952 Pic+kairuki

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki amesema vitendo vya rushwa, urasimu uliokithiri na vinavyoendana na hivyo kwa watumishi wa umma ni chanzo cha kufukuza wafanyabiashara na wawekezaji nchini

Amesema hali hiyo inasababisha kushindwa kufikia lengo la Taifa la ukuaji wa kibiashara.

Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifunga kongamano la kibiashara la nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika lililofanyika kwa siku tatu mjini hapa.

Alisema watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, kwa ufanisi na kuondoa urasimu usio wa lazima ili kuvutiwa wawekezaji.

Kairuki alisema hata kama Serikali ikitumia nguvu kubwa katika kutangaza wafanyabiashara na wawekezaji kuja kuwekeza nchini, kama vitendo hivyo visipokomeshwa watumishi wa namna hiyo wataendelea kuwakimbiza.

Alisema kila mtumishi wa umma anatakiwa ajitathmini katika utendaji wake kwani vitendo hivyo vikiendekezwa vitasababisha wawekezaji kwenda kuwekeza nchi nyingine.

Pia Soma

Alisema Serikali itaendelea kupunguza changamoto ya tozo kwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa lengo la kuboresha biashara.

Naye mkuu wa mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga alisema Serikali haitawavumilia watumishi wa umma mkoani humo watakaokwamisha shughuli za kibiashara kwa wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Rais wa chama cha wafanyabiashara kutoka Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Ndakala Emmanuel alisema mkutano huo uliomalizika usiwe bure, bali Serikali ya Tanzania ifanyie kazi mambo yote yaliyojadiliwa ili kila mmoja aweze kunufaika na makubalianao hayo.

“Kama tusipopata matokeo mazuri ya kikao hiki itakuwa tumekaa bure hapa na kupoteza muda, ila kama mapendekezo yatafanyiwa kazi tutapata mafanikio katika biashara zetu,” alisema.

Hilo ni kongamano la kwanza kufanyika mkoani Kigoma, ambapo baadhi ya mikoa iliyofanya makongamano kama hayo yanayolenga kuvutia uwekezaji ni pamoja Mwanza, Arusha, Lindi na Tabora.

Chanzo: mwananchi.co.tz