Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kairuki aagizo maboresho sekta ya utalii

Kairuki Akerwa Na Kasi Ndogo Ujenzi Wa Madarasa Tabora.jpeg Kairuki aagizo maboresho sekta ya utalii

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki amewataka waandaaji wa maonesho ya Utalii ya Kimataifa ya Swahili (SITE) kuyaboresha zaidi ili kupata washiriki wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Hata hivyo ametangaza tarehe ya maonesho hayo ambayo yatakuwa ya nane kuwa ni Oktoba 11-13 mwaka 2024.

Kairuki amesema hayo wakati akihitimisha maonesho Dar es Salaam na kuwashukuru wadau walioshiriki kwenye maonesho hayo ambapo amesema bila ushiriki wao yasingeweza kufanyika kwa kiwango na ubora mkubwa kama lilivyofanyika.

Vilevile ameipongeza Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kupamba maonesho hayo kwa kuandaa bustani ya wanyamapori hai ambayo imekuwa kivutio kikubwa kwa waliotembelea.

Aidha amewaomba wadau kutoa maoni kuhusu maonesho hayo ambayo yatasaidia kuboresha maonesho ya mwakani na kuyafanya kuwa ya kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live