Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kairuki: Mwendokasi ziende miji mingine

Mwendokasipic Mwendokasi ziende miji mingine

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Verified Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa,(OR-Tamisemi), Angellah Kairuki ameitaka Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) kubuni mikakati ya kuboresha huduma ya usafiri ndani ya Jiji la Dar es Salaam na kupanua wigo wa huduma hiyo katika Majiji mengine yanayokidhi vigezo ikiwemo Arusha, Mbeya, Tanga, Mwanza na Dodoma.

Wito huo ameutoa Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi wa DART na kuwataka kuweka mikakati ya utoaji wa huduma hiyo katika Majiji ambayo yanakidhi vigezo ili kutoa huduma hiyo nchi nzima

Amesema kuwa wakati wa uanzishwaji wa Wakala huo ulikuwa ni kwa Jiji la Dar es salaam lakini bado kuna Majiji mengine ambayo yanatamani kupata huduma ya Mabasi yaendayo kwa haraka, na kuwataka kuweka nguvu kulifanikisha hilo.

Akizungumzia hoja za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG), Waziri Kairuki ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha hoja zote za ukaguzi zinajibiwa kwa wakati na kuzifunga na kuhakikisha hakuzalishwi hoja nyingine.

“Sitegemei tunapoenda kwenye ukaguzi wa mwaka 2021/2022 na kaguzi nyingine mbeleni kupata hoja zinazojirudia wakati mlishajifunza hoja zipi ambazo huwa zinajitokeza wakati kuna wahasibu wabobezi, wakaguzi wa ndani wazoefu na wataalam wengine, hivyo wekeni mkazo kwenye eneo hilo”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live