Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kahawa ya Tanzania kivutio Japan

Kahawa123 Kahawa ya Tanzania kivutio Japan

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kahawa ya Tanzania imeendelea kulishika soko la kimataifa baada ya Kampuni ya ITO EN LTD, ambayo ni kampuni tanzu ya Tully’s Co. Ltd. inayomiliki migahawa maarufu ya Tully’s Coffee, kuzindua aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania nchini Japan katika hafla iliyofanyika jijini Tokyo Machi 14, 2024.

Kahawa hizo ni kutoka mkoa wa Arusha, Tarime mkoani Mara na mashamba ya GDM yaliyoko Mbozi mkoani Mbeya.

Tukio hilo la uzinduzi limefanyika katika Ubalozi wa Tanzania jijini Tokyo likiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Baraka Luvanda na kumshirikisha Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN, Osamu Aizawa, aliyeambatana na wawakilishi wa kampuni hiyo na Kampuni yaTully’s Coffee.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Balozi Baraka Luvanda alizihakikishia kampuni za Japan, uwepo wa mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji wanapoamua kuwekeza katika kilimo au sekta nyinginezo hapa nchini.

Balozi Luvanda amelitaja zao la kahawa kuwa ni miongoni mwa mazao ya kimkakati yanayongoza kwa kulipatia Taifa pato na kuingiza fedha za kigeni.

Aidha, Balozi Luvanda alielezea juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live