Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kafulila: Uchumi wa dunia uanendeshwa kwa mikopo

Uchumi Kupanda Kafulila: Uchumi wa dunia uanendeshwa kwa mikopo

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamishna Idara ya PPP Wizara ya Fedha na Mipango, David Kafulila ametanabaisha juu ya hali ya Ongezeko la Deni katika nchi na Dunia Kwa ujumla.

"Ni dhahiri kuwa mahitaji ya wananchi au watu husika huwa ni mengi na makubwa kuliko Kodi na Mikopo ambavyo unaweza kutekeleza.

"Kwa Takwimu za Uchumi wa Dunia kufikia mwezi wa pili mwaka huu zinaonyesha kuwa ni takribani Dolla trilioni 105, wakati Deni la Dunia liko takribani Dolla za Kimarekani Trilioni 305, na Deni la Serikali zote Duniani ni takribani Dolla trilioni 206

"Hivyo basi Deni la Serikali ni zaidi ya mara mbili kuliko Uchumi wenyewe wa Dunia.

"Sisi angalau Deni letu liko katika asilimia arobaini (40%), na watu wanatazama katika picha hiyo, lakini picha ya Dunia nzima Deni la Serikali zote lipo katika asilimia 226%, na la Dunia ni takribani asilimia 300%" - David Kafulila

Chanzo: www.tanzaniaweb.live