Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KPMG yawafunda washindi kampuni 100 bora

77374 Kpmg+pic

Fri, 27 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katika harakati za kuwezesha ukuaji wa kampuni zinazoonyesha matumaini nchini Tanzania, kampuni ya KPMG Tanzania imewafunda zaidi ya washindi 60 wa shindano la kuzitambua kampuni 100 bora zinazokua kwa kasi nchini Tanzania.

Jukwaa hilo lililofanyika leo Alhamisi Septemba 26, 2019 jijini Dar es Salaam linahusisha washindi wanaounda klabu ya kampuni 100.

Mafunzo hayo hufanyika mara kwa mara chini ya kampuni ya KPMG au wadau wengine kwa kuzingatia mahitaji yanayoonekana kikwazo katika ukuaji wa biashara za washindi za wao.

Meneja wa KPMG, Ian Ngungi amesmea mafunzo hayo yamejikita katika mada inayohusu mbinu za kukabiliana na matishio ya ukuaji wa biashara pamoja na udhibiti wa ndani katika masuala ya usimamizi wa fedha.

Meneja wa miradi, Layla Ghaid amesema mafunzo hayo yamekuwa na matokeo chanya kwa washiriki wenye fursa ya kuchagua maada wenyewe kulingana na changamoto wanazokutana nazo katika uendeshaji wa biashara.

“Hili ni jukwaa,  lengo zaidi ni kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto zao , sasa mafunzo ya leo yanahusisha namna wanavyoweza kuwa na udhibiti wa ndani katika masuala ya fedha, kujikinga na tishio la anguko katika kibiashara.”

Pia Soma

Advertisement

“Inawezekana wadau katika mada ya jukwaa hili wakatoka nje ya kampuni ya Mwananchi Communication ltd (MCL) au KPMG, wakaamua kuwezesha mafunzo kufanyika kwa hiyo tunaamini kabisa itawasaidia kuendelea kukua zaidi katika biashara zao,“ amesema Layla.

Mwaka 2011, Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) na KPMG Tanzania walianzisha shindano hilo yakihusisha kampuni zenye mtaji kati ya Sh1 bilioni hadi Sh20 bilioni.

Vigezo vingine ni kampuni zilizokaguliwa hesabu zake ndani ya miaka mitatu iliyopita hazijaorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na lazima isiwe taasisi ya kifedha, kampuni ya Bima, Saccoss, Kampuni ya huduma za Kisheria au ya ukaguzi.

Costantine Mgimba, Mkuu wa Kitengo cha Ubora katika Kampuni ya uzalishaji wa dawa ya Zenufa, iliyopo Kipawa Jijini Dar es Salaam amesema mafunzo hayo yatakuwa chachu kwa kampuni hiyo kutokana na changamoto zilizopo kwa sasa.

Nassoro Abubakar, mhasibu mkuu wa kampuni ya BQ amesema wakati wanachukua tuzo hiyo walikuwa na mtaji wa Sh4bilioni lakini hadi kufikia mwaka jana kampuni hiyo ilikuwa na mtaji wa Sh10bilioni kutokana na mchango wa mafunzo yanayopatikana kupitia jukwaa hilo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz