Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KCU yaongeza Sh715 milioni mauzo ya kahawa Kagera

Kahawa Pc KCU yaongeza Sh715 milioni mauzo ya kahawa Kagera

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Chama kikuu cha Ushirika mkoani Kagera KCU 1990 Ltd kimetoa Sh715 milioni kwa wakulima wa kahawa hai (organic) katika vyama vya msingi vya ushirika vipatavyo 34 kwa msimu 2022/2023.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 04, 2023 Makamu Mwenyekiti wa KCU 1990 Ltd, Respicius John amesema kuwa, nyongeza hiyo imetokana na ubora wa zao hilo kutoka kwa wakulima, kuondolewa baadhi ya tozo na Serikali na KCU kubana matumizi.

John amesema kuwa, kwa msimu 2022/2023 bei ya kahawa hai (organic) aina ya arabika kilo imeongezwa Sh400 na robusta Sh300 na baada ya nyongeza hiyo arabika imeongezeka kutoka Sh4,900 hadi Sh5,300 na robusta kutoka Sh4,400 hadi Sh4700.

“Chama chetu kimeongeza Sh715 milioni kwa wakulima waliouza kahawa yao kwa msimu wa 2022/203 ambazo ni kilo milioni 2.3 sawa na tani 2,300 ambapo bei imeongezeka kutoka Sh4,400 hadi 4,700 kwa robusta na arabika Sh4,900 hadi 5,300.

“Kuanzia leo April 04, 2023 wakulima wataanza kulipwa nyongeza ya sh 400 kwa kila kilo moja ya kahawa ya arabika na sh 300 kwa kila kilo moja ya robusta,” amesema John.

Amesema kwa msimu uliopita wa 2021/2022 bei ya kahawa hai ilikuwa sawa na bei ya kawaida ambapo kilo moja ya arabika na robusta bei ilikuwa Sh3,400.

Amesema, vyama hivyo 34 vya kahawa hai ni miongoni mwa vyama vya msingi 135 ambavyo vipo katika Wilaya za Muleba, Misenyi na Bukoba na vyama vyote vya msingi 135 vimepata Sh10.8 bilioni kwa msimu wa 2022/2023

Amewaomba wakulima wa kilimo cha kahawa hai hasa ambao wanakiuzia chama kikuu za Kcu kuboresha uzalishaji wa zao la kahawa hasa katika msimu huu wazingatie swala la ubora kwa kuwa ubora ndiyo unasababisha kupata bei nzuri sokoni na kama watafanya hivyo kuzingatia maelekezo wanayopewa na maafisa ughani ambao wameajiliwa na chama hicho ambao wako mashambani itasaidia kahawa ya mkoa wa kagera kupata soko zuri kwenye soko la dunia.

Amesema wakulima wao wamepata fedha itakayowasaidia kusherehekea sikukuu za Pasaka na Eid kufuatia mfungo wa Kwaresma kwa Wakristo na Ramadhani kwa Waislamu

Kwa upande wake Gilbert Makwabe mkulima kutoka Wilaya ya Bukoba amesema fedha hizo zinawafanya wakulima kuwa na motisha ya kuendelea kulima kahawa, kwani walikuwa wameishaanza kukata tamaa.

Chanzo: mwanachidigital