Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji sekta ya madini lililoanza hii leo mkoani Dar es Salaam litakuwa ni sehemu ya kuvutia mitaji ya uwekezaji katika sekta ya madini.
Waziri Mavunde amesema hayo mkoani Dar es Salaam katika Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji sekta ya madini, ambalo linajadili fursa za uwekezaji zilizopo nchini, upatikanaji wa mitaji, matumizi ya teknolojia ya kisasa, ubunifu katika utafutaji, uchimbaji na uongezaji thamini wa madini kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji wa mazingira.
“Aidha mkutano huu utaangalizia masuala ya matumizi ya madini, mkakati kwa ajili ya uzalishaji wa nishati safi”. Amesema waziri Mavunde
Ameongeza kuwa kauli mbiu ya Jukwaa hilo inayosema 'Unlocking Tanzania's Future Mining Potential' imelenga kuweka mazingira yatakayowezesha kuvuna madini yaliyopo Tanzania kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa kizazi cha sasa na kijacho.