Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joto ardhi kuzalisha umeme nchini

Mgao Pic Jotoardhi Joto ardhi kuzalisha umeme nchini

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: mwanachidigital

Shirika la Umeme nchini kupitia kampuni tanzu ya TGDC limeanza kukabiliana na changamoto ya upungufu wa nishati ya umeme kwa kuanza ujenzi wa mradi wa kuzalisha nishati hiyo kwa kutumia joto ardhi (Geothemo) katika hifadhi ya misitu ya asili ya Uporoto wilayani Rungwe mkoani Mbeya ukiwa na uwezo wa kuzalisha megawatI tano.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jafari Haniu, Kaimu Meneja wa huduma za ufundi kampuni tanzu ya Shirika la Umeme nchini TANESCO, TGDC Mhandisi Kenneth Lupogo, amesema umeme wa joto ardhi unazalishwa kutokana na mvuke wa maji yaliyochemshwa chini ya ardhi mvuke huo ukitoka juu unatumika kuzalisha umeme.

Mhamdisi Lupogo amesema mradi huo ambao umeanza kutekelezwa Oktoba mwaka huu karibu na Ziwa Ngosi ni rafiki kwa mazingira kwa sababu mvuke huo unatoka chini ya ardhi na mpaka sasa wapo katika hatua 76 awali 6 kiasi na baada ya kufanya hivyo ndipo wataamua namna kuanza kuzalisha umeme.

Mhandisi Lupogo amesema kuwa umeme wa awali unatarajiwa kuanza kuzalishwa mwaka 2025 kwa kuanza na megawati tano wakati wakiendelea kujihakikishia kiwango cha rasilimali iliyipo uzalisha wa umeme utaendelea kuongezeka.

"Tumeanza kutekeleza mradi huu Oktoba 2023 na tunatarajia kuanza kuzalisha 2025 na tutaanza na megawati tano na kadri rasilimali itakavyokuwa ikiongezeka megawati zitazidi kuongezeka na hii ni jitihada za kutatua tatizo la umeme linaloikabili nchi na hatutategemea tena maji pekee au sola hivyo kutakuwa na joto ardhi," amesema Lupogo Kaimu Meneja ufundi TGDC.

Chanzo: mwanachidigital