Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi thamani ya miamala inavyoshuka

Tozozzzo Jinsi thamani ya miamala inavyoshuka

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya Serikali kufanya marekebisho kwenye viwango vya tozo za miamala ya kieletroniki, thamani ya miamala ya simu kwa mtumiaji mmojammoja wa huduma hizo imezidi kushuka.

Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya robo mwaka unaoishia Desemba 2022 imeonyesha kupungua kwa thamani hiyo kuanzia mwaka 2020 hadi 2022.

Takwimu za ripoti hiyo zinaonyesha mwaka 2020 wastani wa kila mtumiaji wa huduma za kifedha za mitandao ya simu alifanya miamala yenye thamani ya Sh3.96 milioni kabla ya kushuka kidogo mwaka 2021 hadi Sh3.88 milioni na kushuka tena hadi Sh3.44 mwaka 2022. Related

Miamala ya fedha yapanda, Bunge laelezwa Kitaifa Feb 14 2023 Tozo za miamala, mikopo ya wanafunzi ilivyotokisa bajeti Biashara Feb 14 2023

Wastani wa thamani ya miamala hiyo pia umepungua kwa asilimia 11 mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka 2021, sawa na Sh440 bilioni katika kipindi hicho.

Wakati thamani ya miamala ikipungua, pia idadi ya miamala hiyo kwa mtu mmoja imepungua kidogo kutoka 106 mwaka 2021 hadi 102 mwaka 2022, sawa na wastani wa miamala 9 kwa kila mwezi.

Hata hivyo, ripoti hiyo inaonyesha thamani ya miamala kwa ujumla imeongezeka kutoka Sh137.2 trilioni mwaka 2021 hadi Sh140.9 trilioni mwaka 2022.

Takwimu za kushuka kwa thamani ya miamala ya simu zinakuja miezi minne baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba kulieleza Bunge kuwa Serikali imepunguza wigo wa tozo ili kuchochea matumizi ya miamala kwa ajili ya kupunguza fedha taslimu.

“Marekebisho yaliyofanyika ni kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote) na kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki kwenda nyingine,” alisema.

Mwajuma Buremo, mfanyabiashara wa bidhaa mtandaoni alisema amepunguza kufanya miamala ya simu kwa sababu makato bado yanamuumiza na hapati faida kwenye biashara yake.

“Kwa sasa hivi wateja wangu nawaambia wanipatie fedha taslimu, naona wakituma kwa simu makato yanakuwa makubwa na sipati faida kwa sababu mimi mwenyewe ninanunua kwenye maduka makubwa,” alisema.

Vilevile utafiti uliofanywa na taasisi ya GSMA ya Uingereza inayojihusisha na maendeleo jumuishi ya uchumi duniani Desemba 2021, ulioitwa ‘Uchambuzi wa Athari ya Tozo kwenye Miamala ya Simu Tanzania’ ulionyesha watumiaji wengi wa huduma za kifedha za kieletroniki wamepungua kwa sababu ya tozo kupanda.

“(Baadhi) watumiaji wa huduma za kifedha kieletroniki wameacha kutumia njia hizo tangu kuanzishwa kwa tozo, licha ya jitihada za watoa huduma kufanya maboresho ya viwango siku hadi siku,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo.

Mark Patrick ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi alisema ni vyema Serikali ijue kutokana na maendeleo ya Tehama, watu wengi wanafanya miamala kwa njia hizo hivyo wasiweke vikwazo huko.

Hata hivyo, Profesa Humphrey Moshi aliwahiwa kunukuliwa na gazeti hili akisema pamoja na thamani za miamala kushuka, anatatarajia mwenendo ubadilike kwa kuwa huko tuendako matumizi ya miamala ya kielektroniki yatakuwa hayaepukiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live