Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi Royal Tour inavyofungua uchumi wa Tanzania

061b1483e27f52f149de41c57f99e48a Jinsi Royal Tour inavyofungua uchumi wa Tanzania

Tue, 28 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Filamu ya Royal Tour pamoja na ziara za Rais Samia Suluhu Hassan nje ya nchi, zimefungua uchumi wa Tanzania kwa kuongeza uwekezaji kutoka Dola za Marekani bilioni 1 sawa na sh trilioni 2.3 mpaka kufikia Dola bilioni 9.2 sawa na trilioni 21.16.

Pia mauzo ya nje yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 10 sawa na Sh trilioni 23 kutoka dola za Marekani bilioni 7.

Akizungumza katika mkutano wa mafanikio ya ziara ya Rais Samia nchini Oman uliofanyika leo Juni 28,2022 Ikulu, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Godius Kahyarara, amesema kuongezeka kwa mapato hayo ni hatua nzuri, kwani inaongeza watalii wengi na kuongeza mauzo ya nje ambayo yatasaidia kupunguza ukali wa deni la taifa.

Amesema tathmini ya serikali kuanzia Machi 2021 hadi Juni 25, 2022, serikali imeweka lengo la kuongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi na kufikia asilima 30 ya Pato la Taifa (GDP) ifikapo mwaka 2025.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live