Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi Corona ilivyoathiri usafirishaji wa bidhaa nje ya Tanzania

EXPORTATION Jinsi Corona ilivyo athiri usafirishaji wa bidhaa nje ya Tanzania

Wed, 15 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya bidhaa za ndani nchini zimebaki katika vizuizi vya usafirishaji kufuatia mlipuko wa wimbi la tatu la UVIKO-19 licha ya soko la nje kuongezeka thamani katika uuzaji wa bidhaa mbalimbali duniani.

Taarifa iliyotolewa na Benki Kuu, imesema kuwa thamani ya kusafirisha madini ya dhahabu, uzalishaji wa bidhaa zinazotumika katika kukuzia mimea ya bustani zilizo ongezeka kati ya mwezi julai 2021 zimeathirika kufuatia wimbi la tatu la ugonjwa huu.

Taarifa hiyo imesema kuwa usafirishaji wa bidhaa na huduma kwa mwaka 2021 umerekodiwa kufika dola bilioni 8.98 sawa na Shilingi trilioni 185.52 za Tanzania kiasi hiki kinatajwa kuwa pungufu na kile cha mwaka 2020 ambacho kilikuwa trilioni 208.71 za Tanzania.

Walakini usafirishaji wa madini ya dhahabu unatajwa kuongezeka licha ya hali kuw atete katika soko la dunia kufuatia mlipuko wa ugonjwa, soko hilo limekua kutoka dola milioni 261 sawa na shilingi bilioni 605.25 za Tanzania hadi dola bilioni 2.99 sawa na trilioni 4.63 za Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live