Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jiji la Arusha laanza mkakati wa kuboresha mapato

9767 ARUSHA+PIC TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Jiji la Arusha limeanza mikakati ya kuongeza mapato yake ili kuvuka malengo ya mwaka 2018/19 kukusanya Sh15 bilioni.

Akizungumza na MCL leo Alhamisi Agosti 2, 2018 kaimu mkurugenzi wa jiji hilo,  Grayson Orcado amesema tayari wameanza kufanya tathmini upya ya vyanzo vya mapato ili kutekeleza agizo la Rais John Magufuli.

“Mwaka 2017/18 tulikuwa tumejiwekea malengo ya kukusanya zaidi ya Sh13 bilioni, tulifanikiwa kwa kiasi ila kwa sasa tunataka kukusanya Sh15bilioni,” amesema.

Alisema watafanya tathimini ya vyanzo vyote vya mapato na kuona wataviongezaje, “muda huu nipo katika kikao kutazama mambo haya ya mapato hivyo tunaimani ya kufanya vizuri.”

Hivi karibuni meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro alilieleza MCL Digital kuwa makusanyo ya halmashauri yamekuwa madogo kutokana na vyanzo vingi kuchukuliwa na Serikali Kuu.

“Kuna mapato ya kodi ya majengo, mapato ya mabango na mengine kadhaa yanakusanywa na TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania),” amesema.

Amesema Arusha ni kati ya majiji yanayofanya vizuri katika makusanyo yake na wataendelea kufanya vizuri kutokana na kuboresha mifumo ya makusanyo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz