Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Je wajua, Kuweka akiba husaidia utulivu wa akili ?

Akibaaaa Je wajua, Kuweka akiba husaidia utulivu wa akili ?

Thu, 10 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya watu hufikiri kuwa ili uweze kuweka akiba ni lazima uwe na pesa nyingi, kuweka akiba ni kanuni mojawapo ya matumizi mazuri ya pesa.

Ikiwa umekuwa ukipuuza suala la kuweka akiba na kuliona kuwa halina maana Fahamu faida kuweka akiba ya fedha.

Utulivu wa akili Unapokuwa huna akiba yoyote huwezi kuwa na utulivu wa akili. Kila wakati unahofu na wasiwasi juu ya maisha yako, unajiuliza likitokea tatizo itakuaje? Au hitaji fulani linalokuja hivi karibuni litakuwaje?

Unapokuwa na fungu fulani la akiba huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani unajua hata ukikosa fedha akiba yako itakusaidia.

Hukuwezesha kuandaa kesho vyema Maandalizi ya kesho yanafanywa leo. Kuweka akiba maana yake unajiandaa kwa mahitaji ya kifedha ya baadaye yaani kesho. Mtu asiyeweka akiba mara nyingi hafikiri kuhusu kesho wala hana malengo kwa ajili ya baadaye yake.

Hukuwezesha kuwahi fursa Ni mara ngapi umekuwa ukisema au ukisikia kauli kama vile “Ningekuwa na pesa ningenunua hiki kitu”, “Ningekuwa na pesa ningejiunga kwenye hii huduma”, “Ningekuwa na pesa ningejiunga na huu mradi”, n.k.

Hili linadhihirisha kuwa watu hukosa fursa mbalimbali kutokana na kukosa akiba ya fedha. Unapokuwa na akiba ya fedha ni rahisi kuwahi fursa mpya au bidhaa zenye manufaa mara zinapopatikana.

Kujiaandaa kwa dharura Watu wengi huingia kwenye madeni au kupata uhitaji mkubwa wa pesa mara wapatwapo na dharura. Hivyo kwa kuweka akiba utapata faida ya kukuepushia mahangaiko wakati wa dharura kama vile maradhi, msiba, majanga.

Matumizi mazuri ya pesa Kama nilivyoeleza hapo mwanzo kuwa kuweka akiba siyo kuwa na pesa nyingi bali ni maamuzi na mipango stahiki pekee.

Hivyo kuweka akiba kutakufaidisha kwa kukuwezesha kutumia pesa vyema. Ikiwa unapata elfu kumi kwa siku, itakubidi uitumie vizuri ili uweze kutenga fedha ya akiba.

Kama huweki akiba huna haja ya kutumia pesa vyema kwani hakuna sehemu ya akiba inayotakiwa kutengwa.

Uhuru wa kifedha Uhuru wa kifedha ni zaidi ya kuwa na pesa, uhuru wa kifedha ni kuwa mtu ambaye unatakiwa kuwa maishani na kuweza kufanya au kupata kile unachokihitaji maishani.

Hata hivyo pesa ni muhimu sana kwenye swala la uhuru wa kifedha, ingawa pesa hizi zinatakiwa ziambatane na fikra sahihi.

Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kujijengea msingi mzuri wa kifedha ambao ukiambatanishwa na fikra sahihi utakuletea uhuru wa kifedha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live