Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jatu kukusanya bil 7.5/- uwekezaji kwenye kilimo

E97fefd7f60de99d23d0be220c88f02c.jpeg Jatu kukusanya bil 7.5/- uwekezaji kwenye kilimo

Wed, 9 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAASISI ya uwekezaji kupitia kilimo ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini (Jatu) inakusudia kukusanya Sh bilioni 7.5 kwa ajili ya kuongeza uwekezaji na uzalishaji katika kilimo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo ujulikanao ‘Buku 5 inatosha’ unaolenga kuwahamasisha wananchi kununua hisa za taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Peter Gassaya alisema malengo yao ni kuongeza uwekezaji katika kilimo suala ambalo ana amini kuwa ndiyo mwarobaini wa kukabiliana na tatizo la umasikini nchini.

Alisema kwa sasa taasisi hiyo iliyowekeza katika zaidi ya ekari 47 katika mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Morogoro, Pwani, Iringa, inazidi kujiweka vizuri kwa kuangalia fursa za kilimo katika mikoa mingine nchini kikiwamo kilimo cha umwaligiliaji ikiamini ndiyo njia pekee itakayowakomboa Watanzania.

“Kupitia fedha hizo tutakazokusanya kutokana na uuzaji wa hisa na mazao, pia tutaweza kununua zana mbalimbali za kilimo yakiwamo matrekta na kujenga kiwanda cha kuchakata mazao hayo kikiwamo cha kusaga unga hatua ambayo tuna amini itazidi kuongeza mtaji wa taasisi yetu,” alisema Gassaya.

Alisema Jatu yenye wanachama 30 na wateja 70 nchi nzima, inamilikiwa na Watanzania wenye utashi wa kununua hisa za taasisi hiyo na kuwataka wananchi wengi kujitokeza na kununua hisa hizo kwani ndiyo njia pekee yenye uhakika wa kuwaondoa katika umasikini.

Alisema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka 2017 ikiwa na wanachama 12, imeendelea kujipatia mafanikio, suala ambalo ana amini litazidi kuijenga taasisi hiyo na kuzifanya taasisi nyingine kuiga mfano wake.

Chanzo: www.habarileo.co.tz