WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba amesema majaribia ya mitambo ya kufua umeme wa maji katika Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) yatafanyika mwezi Februari mwakani na umeme wa kwanza wa bwawa hilo utaanza kuingizwa katika gridi ya taifa mwezi Juni.
WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba amesema majaribia ya mitambo ya kufua umeme wa maji katika Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) yatafanyika mwezi Februari mwakani na umeme wa kwanza wa bwawa hilo utaanza kuingizwa katika gridi ya taifa mwezi Juni. Akizungumza wakati wa ziara na viongozi wa dini, Waziri Makamba amesema ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 90 na kwamba hadi sasa kiwango cha chini cha maji kinachohitajika kuanza kufua umeme tayari kimeshapatikana.