Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Japan yatoa mabilioni sekta ya uvuvi

90115 Japan+pic Japan yatoa mabilioni sekta ya uvuvi

Sat, 28 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali ya Japan imeipatia Tanzania msaada wa dola 1.818 milioni za kimarekani (sawa na Sh4.2 bilioni kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (Tafico)

Mkataba wa makubaliano kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo umesainiwa leo Ijumaa ya Desemba 27, 2019 ambapo umetajwa kuwa utasaidia kupunguza umaskini na kuwavutia Watanzania wengi kuingia katika uvuvi na kuifanya kuwa shughuli kuu ya kujipatia kipato.

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, kaimu balozi wa Japan nchini, Katsutoshi Takeda amesema kupitia fedha hizo meli kubwa kwa ajili ya uvuvi itanunuliwa ikiwa na vifaa vya kisasa na mashine ya kutengeneza barafu.

“Lakini pia litatengenezwa ghala la baridi kwa ajili ya kuhifadhia samaki, vifaa mbalimbali vya kuvulia samaki na vya karakana vitanunuliwa, gari lenye mitambo maalumu ya barafu na gari la kusambazia samaki vyote vitanunuliwa,” amesema Takeda.

Takeda amesema kutolewa kwa msaada huo ni muendelezo wa yale mazuri ambayo hufanywa na serikali yake kwa Tanzania kupitia sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo, miundombinu, maji na afya.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amesema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo serikali ilikuwa katika mkakati wa kufufua shirika hilo.

Pia kutekelezwa kwa mradi huo utachangia kufikia malengo ya mpango wa Maendeleo wa miaka mitano awamu ya pili (FYDD II) ambao pamoja na mengine unalenga kuboresha sekta ya uvuvi kama shughuli kuu ya kujipatia kipato.

“Mradi huu utaongeza uuzaji wa samaki nje ya nchi, utaongeza uhakika wa chakula nchini, na pia utaboresha thamani na masoko na kupunguza upotevu wa mazao ya samaki baada ya kuvuliwa,” amesema James

Chanzo: mwananchi.co.tz