Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Japan yaahidi kutoa dola bil. 30 kuisaidia Afrika

B2264C3B BF4F 4B6A B11C 61FB73DD8C1E.jpeg Japan yaahidi kutoa dola bil. 30 kuisaidia Afrika

Sun, 28 Aug 2022 Chanzo: eatv.tv

Serikali ya Japan imeahidi kutoa dola za Marekani bilioni 30 ili kuziwezesha nchi za Afrika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kuimarisha utunzaji wa mazingira.

Ahadi hiyo imetolewa jana (Jumamosi, Agosti 27, 2022) na Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida wakati akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Nane wa Kimataifa wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaohusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD8) unaofanyika jijini Tunis nchini Tunisia.

Akizungumza kwa njia ya mitandao wakuu hao kwenye ukumbi wa Palais des Congres, jijini Tunis, Waziri Mkuu Kishida alisema kiasi hicho cha sh. bilioni 30 kitatolewa kwa kipindi cha miaka mitatu ili kuimarisha utunzaji wa mazingira, uwekezaji hasa kwa vijana, sekta za afya, viwanda na elimu.

“Ijapokuwa siko pamoja nanyi kwenye mkutano huo, bado dhamiri yangu ya kuendeleza bara la Afrika iko palepale, haijabadilika. Kwa kuanzia, Japan itaanzisha "Japan’s Green Growth Initiative with Africa" ambapo itatoa dola za Marekani bilioni nne kwa taasisi za umma na za binafsi barani Afrika ili kuziwezesha kutekeleza mpango huo,” alisema.

Alisema Japan imelenga kukuza uwekezaji ambapo safari hii wamelenga kuwainua vijana. Katika awamu hii, alisema watawalenga zaidi vijana wanaoanzisha makampuni na hatua hiyo itawapa fursa vijana wa Afrika na wa Japan kufanya kazi kwa karibu.

Waziri Mkuu KassimMajaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida kwa njia ya mitandao kwenye ukumbi wa Palais des Congres, jijini Tunis.

Kuhusu kuboresha maisha ya Waafrika, Mhe. Kishida alisema kupitia Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) watatoa dola za Marekani bilioni tano ambazo zinajumuisha mkopo mpya wa dola za Marekani bilioni moja zinazolenga kuzisaidia nchi hizo kumudu madeni.

Waziri Mkuu huyo alisema kujitokeza kwa janga la corona kumetoa funzo kuwa kuna haja ya kujiandaa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. Na kwa kuzingatia hilo, Serikali yake itachangia kiasi dola za Marekani bilioni 1.08 ili kuiwezesha Afrika kukabiliana na UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na kuimarisha mifumo ya afya.   

Chanzo: eatv.tv