Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamaa arejea nyumbani kutoka Dubai na kuanza kuuza senene

Senene Jad Jamaa arejea nyumbani kutoka Dubai na kuanza kuuza senene

Thu, 11 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamume mmoja ambaye amerejea nyumbani kutoka Dubai baada ya kufanya kazi kama mpiga rangi, ameanza kuuza senene ili kupata kipato zaidi.

Charles Mukasa mwenye umri wa miaka 34, ambaye alirejea nchini Uganda kwa likizo yake ya mwezi mmoja, alianzisha biashara ya nzige ili kupata kipato zaidi.

Kwenye ripoti ya gazeti la Daily Monitor, Mukasa alisema anataka kupata pesa zaidi kabla ya likizo yake kumalizika ndani ya mwezi mmoja.

Mwanamume huyo anapata Ksh. 366 kwa kila kikombe cha nzige anachouza na Ksh. 29,000 kwa kila gunia la wadudu hao, ambao ni mlo maarufu nchini Uganda.

Mashirika ya Ndege Uganda yatakuwa na kitoweo cha senene katika menyu yao.

Hii ni kufuatia kisa cha hivi karibuni cha mwanamume kunaswa kwenye kamera akiwauza wadudu hao ndani ya ndege iliyokuwa inatokea Dubai kuelekea Uganda hivyo mashirika hayo yanasema yalipata funzo.

Shirika hilo lilisema kuwa wateja wake walifurahiswa na chakula hicho na kuamua kuongeza katika menyu yake kufuatia ombi ya abiria. Kama ilivyoshuhudia na abiria waliotangamana na mchuuzi huyo, kitoweo cha senene kinapendwa sana nchini Uganda.

Wadudu na wanafahamika kwa jina maarufu Nsenene na hata huhifadhiwa na kuuzwa katika maduka kuu na masokoni. Nsenene huwa kwa wingi misumu ya miezi Aprili, Mei, Julai, Oktoba na Novemba.

Wadudu hao waweza kupikwa bila mafuta sababu wana mafuta yao. Nsenenes wanadaiwa kuwa na vitamini A, B, na C na hata kuwa na protini nyingi kuliko maziwa na samaki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live