Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jaji Warioba ashauri utafiti mimea mafuta ya kupikia

13750d75c39b42496f3ef74c7d41ceb0.jpeg Jaji Warioba ashauri utafiti mimea mafuta ya kupikia

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Sua), Jaji mstaafu, Joseph Warioba ameshauri watafi ti wafanye tafi ti za mimea inayoweza kuwa na mafuta yatakayotumika kupikia. Alitoa ushauri huo katika Kampasi ya Edward Moringe alipokuwa akizungumza na watumishi wa Sua baada ya Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda kueleza majukumu ya chuo hicho.

Alisema Tanzania imebarikiwa mimea mingi inayoweza kutoa mafuta ikiwamo alizeti, michikichi, minazi, karanga na mingine ambayo inaweza kuwa na mafuta hayo. “Ukiacha kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol, ilianza mafuta ya kupikia duniani vyanzo vya mafuta haya vilianza kuwa na matatizo,” alisema Jaji Warioba.

Alisema serikali imefanya juhudi kubwa kuendeleza eneo hilo ili taifa lisitegemee mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi. “Serikali inajitahidi kuongeza nguvu kwenye maeneo ya mendeleo, inajitahidi katika kilimo ingawa hali ya sasa ya dunia katika eneo hilo si nzuri na hapa nchini kuna uhaba wa mafuta ya kupikia,” alisema.

Jaji Warioba alisema Sua ina watafiti waliobobea hivyo wachangie mawazo kuhusu namna ya kuendeleza kilimo ili nchi ijitosheleze kwa chakula na mafuta ya kupikia. Katika hatua nyingine, Jaji Warioba alisema serikali inatathmini mfumo wa elimu unaofaa, hivyo Sua ina wajibu wa kuchangia maoni upatikane mfumo wenye manufaa zaidi kwa nchi.

Alisema chuo hicho pia kina wajibu wa kuendelea kutoa elimu itakayosaidia wahitimu kujitegemea na kumudu ushindani kwenye soko la ajira. Jaji Warioba alisema licha ya changamoto zinazokikabili chuo hicho, lakini kumekuwapo na mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ikiwamo uboreshaji wa miundombinu, ukarabati wa majengo ya zamani na ujenzi wa mengine mapya likiwamo la maabara mtambuka kwa kuwezeshwa fedha na serikali.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sua, Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande Othman aliishukuru serikali kwa kutoa fedha za ruzuku zaidi ya Sh bilioni 45.9 kila mwaka na kwa wakati kwa ajili ya kukiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi pamoja na utoaji wa fedha za mikopo kwa wanafunzi zaidi ya 10,800 kila mwaka.

Makamu Mkuu wa Sua, Profesa Chibunda alisema wamekuwa wakifanya vizuri katika miradi ya utafiti inayofadhiliwa na wadau wa ndani na nje yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 25 kila mwaka na kuchapisha nakala kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live