Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jafo atoa taarifa kuhusu biashara ya kaboni

WhatsApp Image 2022 12 16 At 11.jpeg Jafo atoa taarifa kuhusu biashara ya kaboni

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoathirika na athari za mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa isipotabirika.

Waziri wa nchi, ofisi ya Makamu WA Rais - Muungano na mazingira Dkt Selemani Jafo ameyazungumza hayo leo Disemba 16, 2022 Mtumba Dodoma katika mkutano na wanahabari akitoa taarifa kwa Umma kuhusu uzingatiaji na utekelezaji wa kanuni na mwongozo wa biashara ya kaboni.

Dkt Jafo amesema hali hiyo inajidhihirisha kupitia matukio ya mvua zisizotabirika, ongezeko la joto, ukame na mafuriko.

"Athari hizi za mabadiliko ya tabianchi zimeathiri sekta za kijamii na kiuchumi na maendeleo Kama vile kilimo, utalii nishati, maji, afya, mifugo na mifumo ikolojia ya bahari na ardhi, hivyo kuathiri ongezeko la pato la Taifa, ukame wa muda mrefu mrefu na mafuriko pia yamechamgia fharama kubwa za kiuchumi na kuathiri maendeleo na maisha ya jamii za vijijini na mijini," amesema Dkt Jafo.

Aidha Dkt Jafo amesema kuwa biashara ya kaboni ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kukabiliana na mabadiliki ya tabuanchi dunuani.

"Biashara hii hufanyika miongoni mwa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliki ya tabianchi, itifaki ya Kyoto na makubaliano ya Paris Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi mwanachama wa mikataba hii"- Dkt Jafo

Hata hivyo Dkt Jafo amebainisha kuwa pamoja na Sera na mikakati iliyopo na kwa kuzingatia umuhimi wa biaahara hiyo Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeandaa kanuni na muongozo wa Taifa wa usimamizi wa biashara kaboni nchini.

"Malengo makuu ya kanuni na muongozo huo ni kuweka utaratibi na masharti ambayo wadau na wajasiriamali wa biashara ya kaboni watapaswa kuzingatia wakati wakati wa utekelezaji wa miradi mipya na miradi inayoendelea ya biashara UA kaboni katika sehemu mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live