Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jafo atoa mwezi 1 ujenzi skimu ya umwagiliaji

WhatsApp Image 2022 06 18 At 4.06.58 PM.jpeg Selemani Jafo, Waziri wa Mazingira

Sun, 19 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Amechukua hatua wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kwa ajili ya kutembelea na kukagua Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Dk. Jafo alionesha kushangazwa na hali aliyoikuta katika mradi huo unaosimamiwa na wataalamu kutoka Wilaya ya Mvomero wakati serikali ilishatoa fedha zote ili utekelezaji huo ufanyike kwa wakati kama ilivyopangwa.

“Nimekuja kuangalia value for money, sijaridhika na mradi huu wataalamu wametuingiza chaka hatuwezi kuvumulia wataalamu wachache wanaotuvuruga, kwa hiyo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ndani yake wakiwemo TAKUKURU wachunguze mradi huu, tunataka kuona mradi huu unakamilika kwa wakati tufanye kazi kwa maslahi ya wananchi,” alisema.

Hata hivyo, kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa EBARR wilayani humo, alisema mradi huo ulianza kujengwa mwaka 2013/14 umekaa kwa zaidi ya tisa bila kuendelezwa hivyo waliwasilisha ombi Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ilikubali kutoa fedha kiasi cha sh. milioni 710.

Alisema baada ya kupata fedha Mkurugenzi wa Wilaya alituma wataalamu wakague eneo hilo walibaini changamoto liko chini mita moja ukilinganisha na usawa wa mashamba usawa 

“Wananchi wana kiu kuona mradi huu ukikamilika kwa wakati ili uwasaidie kupata majawabu ya mustakabali wa maisha yao sasa hapa tunataka mradi huu iwe mvua iwe jua tutaka uanze kufanya kazi,” alisisitiza.

Aliitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ijipange kununua pampu ya kusukuma maji kwa kuwa wao ndio wasanifu wa mradi huo ili uweze kuanza kufanya kazi kama ilivyotarajiwa.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kisima cha maji safi katika Kijiji cha Mingo wilayani humo ambapo alioneshwa kuridhishwa na utekelezaji wake.

Alitoa maelekezo kwa wataalamu kutoka Wakala wa Maji Mijini na Vijijini (RUWASA) kukamilisha mradi huo Juni 28, 2022 kama walivyomuahidi ili uweze kusaidia wananchi katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Nataka nione maji yanatiririka hapa na kwenda kwa wananchi itakapofika asubuhi ya tarehe 29 mwezi Juni, tunataka kuona wananchi wanafaidika na miradi hii ya mabadiliko ya tabianchi inayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais,” alisema.

Akiishukuru Serikali kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mingo, Rashid Kibukila aliishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuwapelekea mradi huo. 

Mbali ya Mvomero, mradi wa EBARR pia unatekelezwa katika halmashauri za wilaya za Mpwapwa (Dodoma), Kishapu (Shinyanga), Simanjiro (Manyara) na Kaskazini ‘A’ (Unguja).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live