Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jafo: Ongezeni kasi uzalishaji wa sukari

Sukari Zanzibar Jafo: Ongezeni kasi uzalishaji wa sukari

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amekishauri Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo kuongeza kasi ya uzalishaji wa sukari ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo hasa katika kipindi cha mvua ambapo viwanda vingi husimamisha zoezi la uzalishaji kutokana na athari za mvua.

Dkt. Jafo ameyasema hayo leo Septemba 11, 2024 alipotembelea Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo kilichopo Makurunge Bagamoyo Mkoani wa Pwani kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji, kusikiliza na kitatua changamoto zao.

Katika ziara hiyo Waziri Jafo ameushauri uongozi wa kiwanda hicho kuongeza bidii kwenye uzalishaji wa sukari.

“Nchi yetu mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani 802,000 ambayo inajumuisha industrial sugar (sukari ya viwandani) tani 250,000, na ile brown sugar (sukari ya nyumbani) ambayo tunatumia kwa kunywa ni tani 552,000 hivyo nimefurahia uwekezaji huu,” amebainisha Dkt Jafo.

Aidha, Dkt. Jafo amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya sukari nchini kuwa Serikali itaendela kuwalinda na kuwatengenezea mazingira wezeshi ya uwekezaji.

“Rais Samia dhamira yake kubwa ni kuvilinda hivi viwanda kwa nguvu yote na mimi hili jimbo la viwanda ni jimbo langu. Nina majimbo mawili; jimbo la Kisarawe na jimbo la viwanda.”

Aidha Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Frank Nyabundege ametoa msisitizo kwa wazalishaji wa sukari nchini kutosita pale wanapohitaji msaada kutoka katika benki hiyo.

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bakhresa Group, Hussein Sufiani amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha wastani wa tani 1800 hadi 2000 kwa siku na jumla ya wastani wa tani 80,000 zinatarajiwa kuzalishwa na kiwanda hicho malengo yakiwa ni kufikia tani 100,000.

Aidha, kiwanda hicho kinatoa ajira ajira zaidi ya 1500 kwa awamu ya kwanza na kikikamilika awamu zote tatu kitatoa ajira zaidi ya 3000 na kitakuwa na mtambo wa kufua umeme wa Megawati 5 utakaokuwa unatumia taka zinazotoka kiwandani kuzalisha umeme.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live