Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKT kushiriki uchumi wa viwanda

19e74cb8d6dfa06673b0cd59987b502f JKT kushiriki uchumi wa viwanda

Wed, 17 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limeanza mikakati ya kulima mazao ya biashara ambayo yatachangia malighafi ya viwanda hapa nchini.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kimkakati katika kilimo, ufugaji na uvuvi, Kanali Hassan Mabena akiwa katika kikosi cha 844 KJ, Itende, Mbeya ambacho ni miongoni mwa vikosi vinavyolima zao kahawa.

Anasema JKT imeanza maandalizi ya kulima ekari 500 za zao la mkoke katika kikosi cha JKT kilichopo Tanga. " Serikali imeweka mkakati mkubwa kuhakikisha zao la mkonge linazalishwa kwa sababu linakwenda kuwa malighafi katika viwanda vyetu, na sisi JKT tumeliona hilo na kutumia fursa hii."

Kanali Mabena anasema kwa upande wa zao la korosha, JKT imeanza kilimo hicho katika kikosi kilichopo Mtwara na Manyoni mkoani Singida. "Mfano atika kikosi chetu cha Nachingwe tumeshapanda mikorosho 7,300 na tuna mpango wa kuongeza shamba na kupanda miche 15,000 ya mikorosho msimu ujao. kazii kama hiyo inafanyika Singida."

Kanali Mabena anasema kwa upande zao la michikichi wamepanga kulima ekari 2,000 katika kikosi cha 831 KJ na mpaka sasa ekari 700 zimeshapandwa. anasema pia kuna vikosi vya JKT vimeanza kulima zao la alizeti ilikukabiliana na upungufu wa mafuta nchini.

Naye Meja Jenerali, Charles Mbuge alisema kwa msimu wa mwaka huu vikosi vya JKT vimelima ekari 12,247 kwa mazao ya chakula na biashara na kuwa lengo ni kufikia kulima ekari 28,000 ifikapo mwaka 2025.

Chanzo: www.habarileo.co.tz