Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Italia kuanzisha upya safari za ndege Zanzibar

F4e3574ee33dc03405f8b9aaca41cfc4 1140x640 Italia kuanzisha upya safari za ndege Zanzibar

Sat, 11 Jun 2022 Chanzo: dar24.com

Katika kukuza na kuendeleza diplomasia ya uchumi Serikali ya Italia imeahidi kuanzisha upya safari za ndege za moja kwa moja kutoka nchini humo hadi Zanzibar kuanzia Juni 29, 2022.

Ahadi hiyo imetolewa na Inspekta Jenerali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia, Balozi Natalia Quintavalle wakati alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Natalia amesema kuwa kuanzishwa kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Italia hadi Zanzibar zitasaidia sana kukuza biashara na utalii baada ya kusitishwa kwa safari hizo tangu mwaka 2019 kutokana na changamoto ya Uviko 19, na kwamba

Nae Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema kuanzishwa upya kwa safari hizo kutachangia sana kukuza pato la taifa kwani awali kabla ya janga la Uviko 19, Zanzibar ilikuwa inapata watalii 200,000 kwa mwezi kutoka nchini Italia.

Tanzania na italia zimekuwa zikishirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo afya, elimu, utalii, viwanda, maji, kilimo, nishati, pamoja na maendeleo ya sekta binafsi.

Chanzo: dar24.com