Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Israel yatoa tamko sakata la gesi

Gesi Urusii.jpeg Israel yatoa tamko sakata la gesi

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Israel imesema kuwa itakataa marekebisho ya Lebanon kwenye pendekezo lililoandikwa na Marekani la kutatua mzozo wa muda mrefu wa mpaka wa baharini kuhusu eneo lenye utajiri wa gesi katika pwani za nchi hizo za Bahari ya Mediterania.

Rasimu ya makubaliano iliyotayarishwa na mjumbe wa Marekani Amos Hochstein inalenga kutatua madai ya ushindani kuhusu visima vya gesi baharini na iliwasilishwa kwa maafisa wa Lebanon na Israel mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya miaka mingi ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja.

Israel iliyakubali masharti yaliyowekwa na Hochstein na kusema yatatathminiwa kisheria, lakini haikutoa ishara kama itataka yafanyiwe marekebisho. Afisa wa Israel amesema Waziri Mkuu Yair Lapid ameiambia timu ya mazungumzo kuyakataa marekebisho hayo.

Afisa huyo amesema Israel haiwezi kuachia maslahi yake ya usalama na kiuchumi hata kama ina maana hapatakuwa na makubaliano.

Lebanon imesema mazungumzo hayo yamefikia hatua muhimu kabisa ya ama kufanikiwa au kuvunjika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live