Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Indonesia kuendeleza kituo cha kilimo Morogoro

F4H37ZJbYAA6Vz8.jpeg Indonesia kuendeleza kituo cha kilimo Morogoro

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Indonesia, Joko Widodo ameridhia kuendeleza Kituo cha Mafunzo kwa Wakulima Vijijini (Farmers’ Agriculture and Rural Training Centre (FARTC), kilichopo Mikindo mkoani Morogoro ambacho kilianzishwa na Taifa hilo mwaka 1996.

Mbali na hilo, Indonesia imekubali kuisaidia Tanzania katika kilimo cha michikichi, ikiwa ni lengo la Tanzania kuongeza uzalishaji wa mafuta ili kujitosheleza kwa mahitaji ya ndani na kuuza nje ya nchi.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Indonesia, Joko Waidodo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais huyo wa Indonesia yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live