Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

India yatangaza neema kwa zao la mbaazi nchini

India Yatangaza Neema Kwa Zao La Mbaazi Nchini India yatangaza neema kwa zao la mbaazi nchini

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania imeruhusiwa kuiuzia India kiasi cha mbaazi inachoweza kuanzia sasa hadi Machi 2025.

Makubaliano hayo yamefikiwa juzi tarehe 24 Februari 2024 wakati wa mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, na Mwenyeji wake Waziri wa Biashara na Viwanda wa nchini humo Mhe. Piyush Goyal yaliyofanyika jijini New Delhi.

Kadhalika, katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubaliana Tume ya Pamoja ya Biashara kukutana mwezi Aprili 2024, ili kuweka mikakati ya pamoja ya kukuza biashara baina ya Tanzania na India.

Awali kabla ya kufikiwa kwa makubaliano haya, Tanzania iliruhusiwa kuuza kiasi cha tani laki mbili pekee kwa mwaka za mbaazi nchini India.

Waziri Makamba alikuwa nchini India kushiriki Mkutano wa Raisina 2024 sambamba na kufuatilia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini humo mwezi Oktoba 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live