Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idara ya ununuzi na ugavi nchini Tanzania yaonywa

Idara ya ununuzi na ugavi nchini Tanzania yaonywa

Tue, 3 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Naibu Waziri wa Fedha nchini Tanzania, Dk Ashatu Kijaji ameitaja idara ya manunuzi na ugavi kuwa mchwa unaorudisha nyuma juhudi za Serikali.

Dk Kijaji ametoa kauli hiyo leo Jumanne Desemba 3, 2019 wakati akifungua kongamano la 10 la wataalamu wa ununuzi na ugavi waliokutana mjini Dodoma, akisisitiza kuwa rushwa inawaumiza.

Naibu Waziri huyo amesema baadhi ya watu wameshindwa kuisaidia Serikali na Watanzania wanyonge badala yake wanatumia nafasi zao kujinufaisha.

"Mnanunua vifaa feki halafu kwa gharama kubwa, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameliona hilo, mmetia hasara katika maeneo mengi na mabilioni yameteketea bila sababu za msingi," amesema Dk Kijaji.

Amesema hivi karibuni  Sh24.85 bilioni zililipwa kwa mikataba isiyokuwa na hati wakati Sh3.4  bilioni zililipwa bila kushindanishwa kwenye bodi ya zabuni.

Ameitaka bodi ya wakurugenzi kutupia macho ununuzi wa vifaa vya afya kwa maelezo kuwa wananunua dawa zisizokuwa na ubora.

Chanzo: mwananchi.co.tz