Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idadi ya watalii yaendelea kuongezeka nchini

11247 Pic+watalii TanzaniaWeb

Wed, 11 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Idadi ya watalii wanaoingia nchini imeongezeka kutoka 627,325 mwaka 1999 hadi kufikia milioni1.28  mwaka 2016.

Akifungua mafunzo kwa waandishi kuhusu Sekta ya Usafiri wa anga, leo Julai 11, Meneja wa Mamalaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), mkoani hapa, Ludovick Ndumbaro amesema ongezeko hilo  limeongeza na  mapato.

Amesema pato linalotokana na utalii nchini limeongezeka kutoka Dola 0.73  za Marekani mwaka 1999 hadi kufikia Dola  2.1bilioni  za Marekani mwaka 2016.

“Nchi yetu bado ina nafasi kuendelea kuwavutia watalii wa ndani na  nje ya nchi kwa kutangaza vivutio tulivyonavyo,”amesema.

Amempongeza Rais John Magufuli kwa juhudi zake za  kuimarisha na kuboresha sekta ya usafiri wa anga hapa nchini kwa kuunga mkono mradi wa usimikaji wa mfumo wa rada nne za kiraia na kufufua Shirika la Usafiri wa Anga Nchini (ATCL).

Akitoa mada yake ya masuala ya kiusalama, yanayopaswa kuzingatiwa na abiria wa Usafiri wa Anga, Inspekta Mwandamizi Usalama wa Usafiri wa Anga (TCAA), Salim Msangi amesema idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa ndege imeongezeka kwa asilimia 4.8 katika kipindi cha kati ya mwaka 2016/17 na 2017/18.

“Abiria wanaweza kuongezeka zaidi kwasababu ya ujio wa ndege mpya nchini kwa sababu maeneo inayofanya safari yataongezeka,”amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz