Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IMF kuikopesha TanzaniaTsh. trilioni 2.4 kuinua uchumi

IMF MKOPO TZ IMF kuikopesha TanzaniaTsh. trilioni 2.4 kuinua uchumi

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika harakati za kurudisha uchumi baada ya kupigwa vikali na COVID-19, kwa mara nyingine serikali imepokea Tsh trilioni 2.4 ili kurejesha uchumi katika hali yake.

Katika taarifa iliyotolewa na IMF, ilibainika kuwa kukamilika kwa makubaliano haya kumetokana na mikutano kati ya mamlaka ya Tanzania na IMF iliyofanyika kuanzia Mei hadi Juni 2022 huko Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ya IMF, mpango huu unalenga kuendeleza uchumi wa Tanzania. "Uchumi wa Tanzania unaimarika hatua kwa hatua kutokana na athari mbaya za janga la COVID-19 japo mienendo ya vita vya Ukraine vinakwamisha hatua hizo. Msaada wa dharura wa IMF chini ya Kituo cha Mikopo ya Haraka (RCF), na usaidizi wa ziada kutoka kwa washirika wengine wa maendeleo, uliunga mkono juhudi za mamlaka kuongeza mwitikio wa kupambana na athari za janga la Coronaikiw ani pamoja na kuongeza nguvu ya kifedha kuweza kukabiliana na mtikisiko wa kiuchumi" ilisema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo uwekezaji huo utajikita zaidi katika kuinua mitaji, matumizi ya kijami pamoja na kuboresha mazingira ya biashara naushinbdani sambamba na kuimarisha ukuaji wa uchumi imara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live