Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IMF: Ukuaji wa uchumi unadorora barani Afrika

Uchumi Kupanda IMF: Ukuaji wa uchumi unadorora barani Afrika

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti ya Shirika la Fedha la Kimataifa, (IMF) inaeleza kuwa, Waafrika milioni 132 walikabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula mwaka jana na kwamba uchumi wa Kusini mwa Jangwa la Sahara utashuka kwa asilimia 3.6 mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Luc Eyraud, mkurugenzi wa masuala ya utafiti na tathmini ya kikanda katika Shirika la Fedha la Kimataifa, (IMF).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Idara ya utafiti wa IMF sababu kuu za kudorora kwa uchumi ni kupanda kwa mfumuko wa bei, kupanda kwa viwango vya riba, thamani ya juu ya dola ya kimarekani, athari za vita vya Ukraine na kushuka kwa ukuaji wa uchumi wa China.

Kwa mujibu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), uchumi wa dunia unatarajiwa kudorora mwaka huu 2023 kabla ya kuongezeka tena mwaka ujao wa 2024. likitaja sababu za kufunguliwa tena kwa ghafla kwa China baada ya kumalizika IMF inakadiria kuwa ukuaji wa uchumi utakuwa 2.9% mwaka huu na utafikia 3.1% mnamo 2024.

Pierre-Olivier Gourinchas, mwanauchumi mwandamizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa anasema kuwa, "Ukuaji utasalia kuwa dhaifu kwa viwango vya kihistoria, wakati mapambano dhidi ya mfumuko wa bei na vita vya Ukraine vinazikabili shughuli mbalimbali," .

Aidha ameongeza kkuwa, ukuaji wa uchumi ulionekana kustahimili kwa kushangaza katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2022, kulingana na IMF. "Mfumuko wa bei pia unatarajiwa kuimarika, ingawa mfumuko mkuu wa bei, ambao haujumuishi bei tete ya nishati na vyakula, bado haujafikia kilele katika zaidi ya 80% ya nchi," amebainisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live