Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IFCU yamulika fursa soko la ngano

Ngano Ngano IFCU yamulika fursa soko la ngano

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Iringa (IFCU) kimeamua kuhamasisha wakulima wake hasa wanaoishi katika Wilaya ya Mufindi kuwekeza kwenye zao la ngano kutokana na fursa zilizopo.

Kwa sasa asilimia 60 ya ngano inayotumika Tanzania imekuwa ikiagizwa kutoka nje ya nchi hasa Urusi na Ukraine ambako kuna vita.

Meneja wa IFCU, Tumaini Lupola amesema hayo leo Septemba 28, 2022 wakati akiwasilisha taarifa za chama chake kwenye Mkutano wa Wadau wa Kilimo kupitia Kongani ya Ihemi chini ya Taasisi ya kuendeleza kilimo ya Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT).

Amesema hakuna namna ya wakulima kulima kibiashara zaidi ya kutumia fursa za masoko zilizopo.

“Tumeshaanza kutekeleza mikakati ya kulima wetu na nataka niseme wakulima wako tayari kufanya kilimo cha kibishara na hadi mwakani, tutavuna kwa wingi,” amesema Lupola.

Mbali na ngano, Lupola amesema wamefanikiwa kuwasambazia wakulima wa zao la soya pembejeo zenye thamani ya Sh181 Milioni.

Amesema pia wamewasaidia wakulima kupata uhakika wa soko ili wakivuna wasipate hasara.

“Lengo letu ni kuzalisha kwa wingi na kuwasaidia wakulima kufikia soko la uhakika la Soya, tumesha watafuta masoko,” amesema Tumaini.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga alisema lengo kubwa ni kuhakikisha wakulima wanaondoka kwenye umaskini.

“Tunataka wakulima wazalishe kwa tija hata baada ya miradi yetu, wasirudi kwenye umaskini,” amesema Kirenga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live