Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huu hapa mkakati uvunaji gesi asilia

Gesiii Huu hapa mkakati uvunaji gesi asilia

Sat, 9 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gesi asilia iligunduliwa hadi sasa nchini inayofikia futi za ujazo trilioni 57.5 huku sehemu kubwa ikiwa baharini inatarajiwa kuvunwa kupitia mtambo wa kuchakata gesi asilia kuwa kimiminika (LNG).

Akizungumza katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk James Mataragio alisema mradi huo utakapoanza kuvuna gesi kiasi kikubwa kitasafirishwa kwa mauzo ya masoko ya nje na kingine kitabaki kwa soko la ndani.

Alisema hatua za awali za mchakato wa kuanza kwa mradi huo zimeanza kwa kusainiwa makubaliano ya awali na lengo ni ifikapo Desemba mwaka huu makubaliano muhimu na wawekezaji yawe yamekamilika. Kuhusu usambazaji gesi nyumbani, Dk Mataragio alisema wanaendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali itakayosaidia kusambaza gesi nyumbani na kwenye taasisi mbalimbali.

“Upo mpango wa kujenga vituo vitano vya gesi katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Feri, Muhimbili, Kibaha na Ubungo. Vituo hivi tunategemea vitakamilika Machi mwakani na vitasaidia upatikanaji wa gesi asilia,” alisema Dk Mataragio. Alisema uhamasishaji unaendelea kufanywa ili sekta binafsi ijitokeze kujenga vituo vidogovidogo vya gesi asilia kwa sababu ujenzi wa vituo vikubwa unafanywa na TPDC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live