Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hujuma Rea yasababisha hasara Sh40 milioni

Misri Yatangaza Mgao Wa Umeme Kutokana Na Joto Kali Hujuma Rea yasababisha hasara Sh40 milioni

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) umepata hasara ya Sh40 milioni tangu kuanza utekelezwaji wa mradi wa awamu ya tatu, mzunguko wa pili wa kufikisha miundombinu ya umeme katika vijiji mbalimbali mkoani Pwani.

Hasara hiyo ambayo ni sawa na asilimia 10 ya thamani ya mradi, inatokana na baadhi ya watu kuhujumu miradi hiyo kwa kufanya vitendo vya wizi wa vifaa kama nyaya, kuchoma moto nguzo na kuiba mafuta ya transfoma.

Miradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2021 mkoani humo, ukiwa na thamani ya Sh40 bilioni na jumla ya vijiji 402 vimefikishwa huduma hiyo kati 417 vilivyopo mkoani humo, huku vilivyobaki 15.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo Wilaya ya Mkuranga, Mwenyekiti wa Bodi ya Rea, Balozi Jacob Kingu ameiziomba mamlaka za Serikali kuweka nguvu kwenye eneo hilo ili kulinda miundombinu hiyo.

"Miradi una maslahi mapana kwa wananchi hususan wa vijijini kwa sababu nishati ni kila kitu, inawasaidia kwenye huduma za kijamii, vituo vya shule, vituo vya afya lakini pia kuchochea shughuli zao za kiuchumi," amesema Kingu.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy na Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Balozi Jenerali Mstaafu Jacob Kingu (kushoto) wakiwasili katika kijiji cha Kikoo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani leo kukagua utekelezaji wa miradi ya awamu ya tatu ya REA mkoani humo

Kingu ambaye ni Meja Jenerali Mstaafu amesema wizi wa vifaa ikiwemo nyaya na kuchomwa kwa nguzo za umeme, si wa kufumbia macho huku akiomba viongozi wa Serikali ikiwemo serikali za mitaa na jeshi la Polisi kuwasaidia.

"Wananchi wenyeji ambao ni wafaidika wa miradi tunaomba wajitahidi kuongeza nguvu ya kupambana na wahalifu na wakishindwa watoe taarifa," amesema.

Amesema miradi hiyo ina tija kubwa ikiwemo kuongeza fursa za ajira kwa vijana kujiajiri na kuongeza masuala ya kiusalama, huku akieleza kuweka kuharibu miundombinu hiyo iliyojengwa kwa gharama kubwa ni hasara.

Mkazi wa kijiji cha Kikoo, Wilaya ya Mkuranga, Juma Mbwambo amesema wananchi wengi kukosa elimu na kutotambua manufaa ya huduma hiyo ni sababu ya kuendekeza vitendo hivyo.

"Nimuhimu hatua kali zikachukuliwa ili uwe mfano na kwa wengine wenye nia kama hiyo, ili kutengeneza nidhamu na kujali rasilimali za umma," amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa Rea, Hassan Saidy amesema ni muhimu wananchi kuitunza miundombinu hiyo, kwani ipo katika mikoa 25 Tanzania Bara ukitoa Mkoa wa Dar es Salaam.

"Wale wanaoandaa mashamba wahakikishe wanakuwa waangalifu wasichome moto nguzo, lakini unaweza kuona nguzo imelalia laini toa taarifa ili mkandarasi aje kufanya marekebisho," amesema.

Amesema kasi ya wananchi kujitokeza kuunganishwa na huduma ya umeme wa Rea kwa baadhi ya vijiji bado ni ndogo, huku akieleza kila kijiji kinachoingiziwa wananchi 66 wanaunganishwa kwa bei ya Sh27,000 baada ya Serikali kulipa gharama nyingine.

"Lakini katika kijiji hiki cha Kikoo hapa Mkuranga, ni wananchi 20 tu wamejitokeza kulipa kiasi hicho cha kuunganishwa, natoa rai kwa wananchi wengine kujitokeza kulipia ili waunganishiwe, kwani wakandarasi wakitoka fursa hiyo haitakuwepo tena," amesema

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Ally amesema umeme katika wilaya hiyo ni muhimu kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa.

"Wawekezaji wa viwanda wapo 248, lakini viwanda vikubwa wapo 109, wilaya ina vijiji 125, kuna vijiji vichache havijafikiwa na huduma kutokana na changamoto ya kufikika kimiundombinu hususan visiwani," amesema.

"Serikali tuna mpango wa kuinua shughuli za utalii katika visiwa vile na tuko kwenye hatua mbalimbali kualika taasisi nyingine ikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kupata kiwanja tuweze kufungua fursa," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live