Programu zilizobainika kuwa sehemu ya ulaghai huo ni za Afya, Michezo na za Kuhariri Picha, ambapo huwahitaji Watumiaji kuingiza taarifa za akunti zao za Facebook.
Taarifa kutoka mtandao huo zinasema walibaini Apps zaidi ya 400 za udukuzi kwenye Play store ya Google inayotumiwa na vifaa vya Android na App Store ya vifaa vya Apple zinazoiba Taarifa Binafsi za wateja.
Msemaji wa META, Gabby Curtis ametaja taarifa zinazohusishwa na udukuzi ni pamoja na Majina ya watumiaji na Nywila (Passwords), hivyo wameshauri wateja duniani kote kuhakiki taarifa za usalama wa akaunti zao.
Google imesema programu zilizobainika kuwa sehemu ya ulaghai huo ambazo ni za Kuhariri Picha, Games, Afya na zinazohusu Mitindo ya Maisha tayari zinaondolewa kwenye Google Play Store.