Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma zarejea Hoteli White Sands

15170 Pic+whjite TanzaniaWeb

Sun, 2 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya sehemu kubwa ya hoteli ya Whitesand ya jijini Dar es Salaam kuteketea, huduma katika hotelini hapo zinaendelea kama kawaida.

Moto huo uliozuka juzi majira ya saa kumi jioni uliteketeza jengo lote la utawala lenye sehemu ya baa, jiko, ukumbi wa mikutano, mapokezi na vyumba vinne vya kulala.

Akizungumza na gazeti hili jana, msaidizi wa mkurugenzi wa hoteli hiyo na msemaji wa kampuni ya Whitesand, Abubakar Mlawa alisema huduma zinaendelea kama kawaida na ulinzi umeimarishwa.

Mlawa alisema majira ya saa kumi jioni wakiwa kazini moto ulizuka ghafla wafanyakazi wa hoteli waliokuwa wakijitahidi kuuzima lakini kutokana upepo mkali ulisambaa kwa kasi hivyo uliwashinda.

Kuhusu hasara waliyoipata, Mlawa alisema ni kubwa kutokana na vitu vilivyokuwa ndani ikiwamo vinywaji, kompyuta na samani nyingine za ndani huku baadhi yake vikiibwa.

Juzi kikosi cha zimamoto na uokoaji kilieleza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo alisema matukio ya moto husirikiana na vikosi mbalimbali na uchunguzi utakapokamilika taarifa rasmi itatolewa.

Chanzo: mwananchi.co.tz