Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma zaendelea hoteli ya Whitesand

15023 Jengo+pic TanzaniaWeb

Sat, 1 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya sehemu kubwa ya hoteli ya Whitesand ya jijini Dar es Salaam, kuteketea kwa moto huduma katika hoteli hiyo zinaendelea kama kawaida.

Moto huo uliozuka jana majira ya saa kumi jioni na uliteketeza jengo lote la utawala lenye sehemu ya baa, jiko, ukumbi wa mikutano,mapokezi na vyumba vinne vya kulala.

Akiongea na MCL Digital leo Jumamosi Septemba mosi msaidizi wa Mkurugenzi wa hoteli hiyo na msemaji wa kampuni ya Whitesand Abubakar Mlawa amesema huduma zinaendelea kama kawaida na ulinzi umeimarishwa.

"Jengo lililoungua ni jengo la utawala ambalo kuna mapokezi, baa, jiko,ukumbi wa mikutano,chumba cha mazoezi na vyumba vinne vya kulala wateja" amesema  Mlawa.

Kuhusu chanzo cha moto amesema majira ya saa kumi wakiwa kazini moto ulizuka gafla kutokana upepo kuwa mkali ulisambaa kwa kasi na kusababisha kikosi cha hoteli kuzidiwa.

"Moto ulizuka kwa kasi ndani ya muda mchache na tukalazimika kuomba msaada kwa vikosi binafsi na vikosi kutoka jiji na kufanikiwa kuuzima saa mbili," amesema.

Kuhusiana na hasara walioipata amesema hasara ni kubwa kutokana na vitu vilivyokuwa ndani ikiwemo vinywaji,kompyuta na samani nyingine za ndani pamoja na kuibiwa baadhi ya vitu.

"Hasara ni kubwa hadi sasa siwezi kusema ni kiasi gani lakini kikosi cha zimamoto na watu wa bima wameanza uchunguzi ukikamilika tutaekeza chanzo na hasara" ameongeza.

 Jana kikosi cha Zimamoto kilieleza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz