Dar es Salaam. Katika kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia watanzania wengi bila kujali kiwango chao cha elimu Benki ya NMB imeziweka huduma zake katika lugha ya Kiswahili.
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni mpya ya benki hiyo ya kuhamasisha matumizi ya digitali katika kupata huduma za kibenki.
Ofisa Mkuu wateja binafsi, biashara ndogo na za kati Filbert Mponzi amesema kampeni hiyo inayofahamika kama ‘NMB Mkononi’ inalenga kuwafanya watanzania wa mijini na vijijini kutumia simu za mkononi kupata huduma za kibenki.
Mponzi ameeleza kuwa kupitia kampeni hiyo wateja wao wenye simu za mkononi hawatakuwa na ulazima wa kwenda kwenye matawi kwa ajili ya kupata huduma kwani kila kitu kinaweza kufanyika kwenye simu.
Kuhusu kutumia Kiswahili amesema utafiti umeonyesha kuwa asilimia 60 ya watumiaji huduma hawana uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya kiingereza hivyo wameona ni vyema kuwasogezea huduma zao kwenye simu za mkononi kwa kutumia lugha inayoeleka kwa watanzania wengi.
“Hivi karibuni tumetoka kwenye mkutano wa SADC na lugha ya Kiswahili imepitishwa lugha rasmi mawasiliano, upande wetu tukaone tushiriki katika kuitangaza lugha hii na ndiyo maana tumesowasogezea watanzania hasa walioko vijijini waweze kupata huduma za kibenki kwa luga wanayoielewa,”
Pia Soma
- VIDEO: Warioba: Vita ya rushwa inakwepa viongozi
- Mahakama imemuachia huru aliyekuwa makamu wa Rais wa TF Michael Wambura
- VIDEO:Majaliwa aagiza watumishi watatu walioajiriwa ‘kindugu’ kuondolewa kazini