Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma za bandari kidijitali Tanzania rasmi mwaka 2021

Huduma za bandari kidijitali Tanzania rasmi mwaka 2021

Wed, 15 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2021 huduma zote za bandari nchini Tanzania zitaanza kutolewa kidijitali.

Mteja ataweza kutumia simu yake ya mkononi au kompyuta kujaza taarifa mbalimbali za kusafirisha au kuagiza bidhaa.

Leo Jumatano Januari 15, 2020 Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema zimeanza kutolewa lakini hadi Desemba 2021, kila huduma itatolewa kidijitali na mteja anaweza kufuatilia mzigo wake akiwa sehemu yoyote.

Akizungumza leo katika mkutano wa wadau wa bandari mkurugenzi mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko amesema bandari za Tanzania zinaboreshwa kuwa za kisasa ili kutoa huduma bora.

“Bandari ya Dar es Salaam tunataka iwe kubwa kwa kuwa ndio  lango la Afrika. Uboreshaji wa miundombinu ya bandari unachagiza kasi ya uwekezaji nchini, kukua kwa biashara na kushamiri kwa viwanda,” amesema Kakoko.

Anasema hakuna mashindano katika huduma za bandari na kwamba bandari zilizopo Afrika Kusini hadi Djibuti hazina uwezo wa kuihudumia Afrika kikamilifu.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema shughuli za bandari ni muhimu katika kukuza biashara, ndio sababu Serikali uboreshaji.

“Tunafanya uboreshaji wa bandari ili zihudumie meli kubwa zaidi,  pia kuna uboreshaji wa reli za kisasa na reli za kawaida, barabara na shirika la ndege ili kuinua sekta ya uchukuzi,” amesema.

Amesema baada ya uboreshaji huo kukamilika, gharama za kufanya biashara zitapungua na ufanisi utaongezeka kupitia teknolojia.

Chanzo: mwananchi.co.tz