Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huduma za Uber yarejea tena nchini

Uber Pic Data Huduma za Uber yarejea tena nchini

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya usafiri kwa njia ya mtandao ya Uber imerejesha shughuli zake nchini Tanzania baada ya kusimamishwa kazi kwa miezi tisa.

Kampuni hiyo ililazimika kusitisha huduma nchini kufuatia mabadiliko ya udhibiti wa usafirishaji yaliyofanywa na Serikali chini ya Wakala wa Usafiri wa Nchi Kavu LATRA yaliyoanza Aprili, 2022.

Uber ilisitisha shughuli zake mnamo Aprili 14, 2022huku ikitaja mabadiliko hayo kuwa chanzo cha usitishwaji wa huduma hiyo kwani hayaendani na uhalisia wa soko la Tanzania.

Kulingana na kampuni hiyo, ilibaini kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) imeunda sera kali za udhibiti ambazo zilifanya uendeshaji wa biashara nchini kutowezekana.

"Tumefanya uamuzi mgumu wa kusitisha huduma zetu nchini Tanzania kuanzia Alhamisi tarehe 14 Aprili 2022. Nauli elekezi iliyowekwa na LATRA imeleta changamoto kubwa kwa mifumo kama Uber kuendelea kutoa huduma kwa wateja wetu," kampuni hiyo ilisema katika taarifa yake.

Kurejea kwa huduma hizo kulionekana siku ya Jumatano katika programu ya Uber, ambapo sasa mteja anaweza kuomba usafiri iwe gari, Bajaji na pikipiki popote pale.

Uber haijatoa taarifa yoyote inayosema sababu ya kuanza tena.

Mwezi huu Latra ilitangaza mwongozo mpya wa nauli ambao uliruhusu kampuni kutoza hadi asilimia 25 ya kamisheni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live