Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hoteli za kitalii za Ngurdoto, Impalla kupigwa mnada

50346 Pic+hotel

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Hoteli  maarufu za kitalii mkoani Arusha, Impalla na Ngurdoto Mountain Lodge zimetangazwa kuuzwa na Benki ya Exim (T) Limited.

Hoteli hizo ambazo zinamilikiwa na wafanyabiashara kadhaa nchini, ambapo Mkurugenzi wake Mkuu, Melau Mrema alifariki mwaka 2017 zinauzwa na kampuni ya uwakili ya Locus ya  jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa matangazo ya kuuzwa hoteli hizo, mnunuzi anatakiwa kutuma zabuni kwa kampuni hiyo kupitia wakili Dk Onesmo Kyauke kabla ya April 15 mwaka huu.

Hata hivyo, mmoja wa wakurugenzi wa benki hiyo, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake alisema hana taarifa za hoteli hizo kudaiwa na Exim Bank.

"Tumeshangazwa na hili tangazo, sisi Exim hawatudai tunadaiwa na NBC bank ambao ndio wana hati zetu na leo nimewauliza kuhusu deni hili nao wameshangaa" alisema.

Hata hivyo, alisema wanafuatilia kujua chanzo cha tangazo hilo ambalo pia linataja viwanja viwili vya Impalla hoteli.

Hata hivyo, Dk Kyauke  alipotakiwa kuelezea juu ya tangazo hili alijibu  kwa ujumbe wa simu yupo mahakamani.

Katibu mtendaji wa chama cha wamiliki wa kampuni za Utalii Tanzania (TATO), Sirili Ako alipotakiwa kuelezea juu ya tangazo hilo alisema ameliona lakini wao wanachohitaji ni watalii kupata huduma bora.

"Nimeona Tangazo TATO hatuhusiki kufuatilia umiliki wa hoteli sisi tunataka watalii wapate huduma bora" alisema.

 Hoteli za Impalla na Ngurdoto ni maarufu sana nchini kwani zimekuwa zikipokea watalii na mikutano mikubwa ya kimataifa.

Lakini siku za karibuni mikutano imepungua ambapo pia mikutano ya Serikali inafanyika kumbi za Serikali.

Ngurdoto Mountain lodge ilipata umaarufu serikali ya awamu ya tatu na nne kwa kupokea mikutano mingi ikiwapo mikutano ya semina elekezi.



Chanzo: mwananchi.co.tz