Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Homera awaamsha wajasiriamali kuchangamkia fursa SADC

Mafunzo Pic Data Homera awaamsha wajasiriamali kuchangamkia fursa SADC

Sat, 21 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema wakati Serikali mkoani humo ikitarajia kuanza kupokea mafuta kutoka Bandari kavu ya Malawi, wafanyabiashara na wajasiriamali wajiandae kutumia fursa hiyo kupanua wigo wa shughuli zao na kufikia nchi zilizopo kwenye Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Homera amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wafanyabiashara na wajasiliamali kutoka sekta binafsi na za umma iliyoandaliwa na mradi wa Markup chini ya kituo cha kimataifa cha biashara (ITC) yenye lengo la kuongeza thamani, kupunguza changamoto na kutumia fursa.

Amesema kwa sasa Mkoa wa Mbeya utaanza kupokea mafuta kutoka bandari kavu ya Malawi, akisema hatua hiyo itaongeza tija kwenye shughuli za kibiashara baina ya Tanzania na nchi hiyo jirani.

Pia ameeleza kuwa wanatarajia kufufua bomba la mafuta la nchini Zambia ikiwa ni mkakati wa serikali ya awamu ya sita kufungua fursa kuzifikia nchi za SADC na kwamba ni muda muafaka watanzania kunufaika na shughuli zao za kibiashara.

"Mkakati uliopo kwa sasa ni kuboresha miundombinum ambapo hivi karibuni tutaanza ujenzi wa barabara nne kutoka Uyole kupita Mlimanyoka hadi Ifisi, ttumie fursa hizi" alisema Homera.

Kwa upande wake mfanyabiashara, Olais Olaseenga alisema kutokana na mafunzo hayo wanaamini yatawabadilisha kifkra na kuweka ushindani kama walivyo wenzao katika mataifa ya nje ikiwamo Kenya ambao wanaonekana kuteka zaidi soko.

"Tunaamini mafuzo haya yanaenda kutusaidia kutuamsha zaidi kwenye kuongeza mnyororo wa thamani katika biashara zetu kushindana na wenzetu kama Kenya, kimsingi ni kutengeneza mahusiano na uhusiano " amesema Olaseenga.

Naye mratibu wa mradi wa Markup, Safari Fungo alisema lengo la mafunzo hayo ilikuwa ni kuwajengea uwezo wafanyabiashara kupata masoko Afrika mashariki lakini kuwaunganisha sekta binafsi na umma ili kupunguza changamoto na kutumia fursa.

"Kwanza wataweza kuboresha mazingira ya biashara lakini kujadili vigezo vya kibiashara ambavyo siyo vya kikodi bali kiforodha, matarajio yetu ni kuona tunapiga hatua kama Taifa katika sekta hizi na kukuza uchumi" amesema Fungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live