Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi hapa sababu za kupanda kwa bei ya vyakula vya mifugo

Animal Pic Hizi hapa sababu za kupanda kwa bei ya vyakula vya mifugo

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuongezeka kwa mahitaji ya maharagwe ya soya nchini China kumesababisha kupanda kwa bei ya chakula cha mifugo hali iliyopelekea wazalishaji wa vyakula hivyo kutumia masalia ya dagaa kama mbadala.

Bei ya chakula cha kuku aina ya 'bloire' kwa kilogramu 50 imepanda kutoka shilingi 68,000 hadi 75,000 kwa kipindi cha miezi miwili, haya yakitajwa kama matokeo ya kuongezeka kwa gharama za maharagwe hayo nchini Malawi na Zambia maeneo mbayo wazalishaji wa vyakula vya mifugo nchini huchukulia malighafi hiyo.

Matokeo ya uhaba huu umepelekea uzalishaji wa mifugo hiyo kupungua kwa kasi sana kwani wafugaji wengi wameshindwa kumudu gharama za chakula.

Hata hivyo Wazalishaji wa vyakula hivyo wametoa ombi kwa Serikali kufungua mipaka zaidi ili maharagwe hayo yaingie nchini kwa wingi na kwa bei rahisi kwani kwa miaka yote walitegemea masoko ya nchini Zambia na Malawi.

Kufutia kilio hicho Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe,amesema kuwa ;

"Serikali haitaweza kuzuia usafirishaji wa bidhaa hii nje ya nchi, kwani kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa hii kunapaswa kuwafanya wakulima kuongeza uzalishaji, na kupitia usafirishaji huu ieleweke kuwa Serikali inakusanya mapato pia" Amesema Bashe.

Ameongeza kusema kuwa katika juhudi za kuongeza uzalishaji wa zao hilo Serikali inaandaa mazingira rafiki kwa kutengeneza mikataba itakayo waruhusu wafugaji kuingia mikataba na wakulima ili kuweza kupata malighafi hizo mapema.

Pia Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa mbegu za zao hilo zinapaikana kila wakati, kuandaa maeneo ya vitaru hasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara, na kuwa tayari watafiti wapo kazini kufanya uchunguzi wa kina kuhusu udongo wa maeneo hayo ili kufahamu kama utafaa na kukidhi mahaitaji.

Na kwa mujibu wa tafti zilizofanyika mwaka 2018/2019 zinaonesha kuwa uzalishaji wa zao hilo umeongezeka kwa asilimia 7.7 kwa tani 22,953 huku wazalishaji wakubwa wakitoka mikoa ya Ruvuma, Morogoro, Iringa, Mbeya na Rukwa.

Kwa mujibu wa tafiti ziliofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, mwaka 2020/2021 zinaonesha kuwa uzalishaji wa kuku nchini umeongezeka kutoka milioni 833.8 hadi 88.7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live