Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula amezitaja faida hizo leo Agosti 4, 2023, wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa soko la Madini ya Tanzaniate katika Mji Mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara.
"...uwepo wa soko hili, utatufanya pia tujulikane zaidi, na soko ambalo litakalibisha hata watu wa nje, tunaimani na wale wafanyabiashara sasa, ili kuweza kuilinda lrasilimali ya nchi, kuweza kuhakikisha kwamba 'exporter' mkubwa, wa madini ya Tanzanite ni yule yule ambaye yanatokana kwenye nchi yake, pamoja na kuwa na soko hili," amesema Waziri Mabula.
Ujenzi wa mradi wa soko hilo unatekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) chini ya mshauri Chuo cha Ufundi Arusha kwa gharama ya Sh5.49 bilioni.
Awali Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mkoa wa Kilimanjaro, Juma Kiaramba, alimueleza Dk Mabula kuwa, ujenzi wa soko hilo ulianza rasmi Mei 22, 2022 na kwamba unatarajia kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu.