Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo jinsi TARI ilivyomkosha Rais Samia

Df65775bc4ea70bc22777d5a6888d732 Hivi ndivyo jinsi TARI ilivyomkosha Rais Samia

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan, amewapongeza watafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kwa kazi kubwa wanazofanya.

Rais Samia ametoa pongezi hizo baada ya kupata maelezo kutoka kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, wakati alipotembelea banda la Wizara ya Kilimo, katika kilele cha maonesho ya kitaifa ya wakulima yanayofanyika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.

Waziri Bashe amemweleza Rais Samia kuwa Wizara inajenga uwezo TARI, kupitia Kituo cha Mlingano, ili kufanikisha ukusanyaji wa sampuli za udongo nchi nzima na kuzipima katika maabara, ili kubainisha afya ya udongo na kuwashauri wakulima juu ya watumizi ya mbolea na kuzalisha kwa tija.

Kuhusu kukabiliana na uhaba wa mafuta ya kula, Bashe amemueleza Rais Samia kuwa wizara kupitia taasisi za TARI, ASA na TOSCI, itazalisha mbegu bora za alizeti tani 5000, ambazo zitasambazwa kwa wakulima.

Hatua hiyo itawawezesha wakulima kuzalisha alizeti nyingi, ambayo itakamuliwa na kuongeza upatikanaji wa mafuta ya kula nchini.

Akizungumzia utafiti, Bashe alimwelezea Rais kuwa serikali yake imeongeza bajeti ya utafiti kutoka Sh bilioni 11 hadi bilioni 40 kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.

Alisema fedha hizo zitatumika kuongeza upatikanaji wa mbegu bora kwa mazao mbalimbali nchini.

Akizungumzia upatikanaji wa Mbegu bora za mahindi, Waziri Bashe alimweleza Rais Samia kuwa, wizara inaweka nguvu kuhakikisha mbegu bora ya mahindi ambayo ni chotara UH6303 inayofaa kwa ukanda wa Nyanda za Juu Kusini itazalishwa kwa wingi, iweze kusambazwa katika ukanda huo.

Waziri alisema jitihada zinaendelea kuhakikisha mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na TARI zinazalishwa na ASA, ili ziweze kupatikana kwa wakulima.

Waziri Bashe pia alimjulisha Rais Samia kuwa, ili kuwa na vyanzo vya nasaba za utafiti wakati wote, Wizara imeanza kukusanya na kuhifadhi mbegu za asili zisipotee kwa matumizi ya sasa na ya baadae.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live