Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo jinsi China itakavyo athiri uchumi wa Tanzania

China Pic Hivi ndivyo jinsi China itakavyo athiri uchumi wa Tanzania

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni dhahiri kuwa China ipo mbali sana kiuchumi kuliko Tanzania, lakini kwa hali inayoendelea sasa katika bara la Asia kufuatia mtikisiko mkubwa kiuchumi uliozikumba nchi nyingi barani humo hali yaweza badilika kwa taifa hilo nguli duniani.

Wataalamu wa masuala ya uchumi wanaona hali hiyo kuwa inaeza kuathiri uchumi wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Afika kwa ujumla kwani nchi nyingi barani humu zinategemea uchumi wa china kwa kiasi kikubwa.

Hii inatokana na Uchumi wa China kushuka zaidi katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2021 tofauti na mategemeo ya wengi duniani.

Taifa hilo ambalo ni la pili kwa uchumi duniani baada ya Marekani, limeshuka kwa kasi kufuatia athari za ugongwa wa Corona.

Kwa mujibu wa kituo cha Utafiti cha taifa nchini humo cha NBS, kimeeleza kuwa uzalishaji wa bidhaa za ndani umeongezeka kwa asilimia 4.9 pekee kwa mwaka 2021.

Msemaji wa NBS, Fu Linghui amewaambia waandishi wa habari kuwa;

"Mazingira ya biashara kimataifa hayajakaa sawa, vilevile bado uchumi wa ndani wa taifa haujaimarika"

Uchumi wa taifa hilo umekuwa kwa asilimia 0.2 pekee kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita ukuaji huu umetajwa kuwa dhaifu kuliko ule wa mwaka 2020.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi nchini Tanzania wamesema kuwa China ni moja kati ya vyanzo vikuu vya uwekezaji wa kigeni nchini'Foreign Direct Investment FDI' hivyo kushuka kwa uchumi wake kutaathiri kwa kiwango kikubwa uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Miaka michache iliyopita China alikuwa muwekezaji mkubwa wa kigeni nchini Tanzania, akiyapita mataifa mengi ya Magharibi kwa kuwa na wawekezaji wenye uthubutu wa kweli katika kutafuta masoko mapya ya nje.

Takwimu zinaonesha kuwa toka mwaka 1990 hadi 2017 China ilikuwa ikiongoza kwa umwekezaji wenye thamani ya dola bilioni 5 sawa na trilioni 11.5 za kitanzania.

Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Abel Kinyondo amesema kuwa ukuaji hafifu wa uchumi wa China sio jambo zuri kwani kwa miongo mingi iliyopita taifa hilo limekua likiendesha uchumi wa dunia kwa kutoa mikopo, misaada pamoja na kuwekeza kwenye maboresho ya miundombinu hasa ya Afrika.

Kushuka kwa uchumi huo kutapeleka kundi kubwa la watu kukosa ajira, mapato ya taifa kushuka, kuzorota kwa ukuaji a teknolojia sambamba na kupungua kwa uwekezaji wa kigeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live